MAPENZI




"Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha.

Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu.

Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tutumie kinga lakini aliipinga sana.
Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanyaalivyotaka. Kwa mara yakwanza nika toa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.

Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi.

Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto.

Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijuatayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia.

Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulishanyumbani na alitaka kunioa. Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.

Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa.Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia baruahii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu.

Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyikanakufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibayamaana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!

Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako

No comments:

Post a Comment