WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA KITUO CHA MPITO CHA WAKIMBIZI MJINI KIGOMA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiwa ndani ya moja
ya nyumba za Wakimbizi waliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi
(NMC) kilichopo mjini Kigoma. Katika nyumba hiyo Waziri Chikawe
alizungumza na familia ya mkimbizi kutoka nchini Kongo (kushoto)
wanaoishi katika nyumba hiyo. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa
ziara ya kikazi. Wapili kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Kituo hicho
kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo
wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya
kiusalama, na waomba hifadhi ya muda ya ukimbizi. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiangalia jiko
ambalo linatumika kupikia chakula cha wakimbizi katika Kituo cha Mpito
cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Katikati ni Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo
hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400
wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye
matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi ya muda ya ukimbizi. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimsalimia mkimbizi
kutoka nchini Kongo aliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC)
kilichopo mjini Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake wapo mkoani
Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo
kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu,
wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi
ya muda ya ukimbizi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwasalimia
waimba kwaya wakimbizi kutoka nchini Kongo waliopo katika Kituo cha
Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Waimba kwaya hao
walimpokea Waziri Chikawe kwa nyimbo mbalimbali wakati alipotembelea
Kituo hicho cha mpito. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri
Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo
mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda
kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na
waomba hifadhi ya muda ya ukimbizi. Picha zote na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment