UHARAMU WA ‘SIKU YA WAPENDANAO’ (VALENTINE’S DAY)
Katika
nchi zote za Ki-magharibi na nchi za Waislamu kwa kuigiza wamagharibi
tayari kauli mbiu ya “acha msimu wa mapenzi uanze” inaanza kusikika
tena. Ni wakati kama huu wa mwezi wa Februari ya kila mwaka ambapo maua
husambazwa, wapenzi hupeana stika, kadi za mapenzi, hutumiana sms za
mahaba, kukiri makosa ya kimapenzi na kupeana miadi mipya (ambayo ni
nadra mno kutekelezeka).Yote hayo kwa lengo la kuchapua mapenzi baina ya
wapendanao katika ‘Siku ya Wapendanao’ (Valentines’Day) Siku
ya Februari 14 ya kila mwaka inajulikana kama ‘Siku ya Valentine’
inayonasibishwa ati ni ‘Siku ya wapendanao’. Ni siku ambayo kwa karne
nyingi imeandaliwa maalum kuwatukuza wapendanao. Katika siku hiyo kadi
hufurika kwa watu kutuma ujumbe wa “penzi la kweli (true love)” kwa
wanaowapenda. Watoto nao pia huwamasishwa kuitukuza siku hiyo ya
Valentine, na hata wanapokuwa katika viwanja vya michezo huhimizwa
kuwaonesha mapenzi ya udhati kwa watoto wenzao wanaowapenda. Jee kuna
madhara gani kusherehekea siku hiyo? Anaweza mtu kuuliza, kwa kuwa
mwisho wa yote, hii ni siku ya kuwaonyesha hisia zako jinsi gani
unamjali na unavyowapendampenzi wako na kwa watoto huwa ni kama
kujifurahisha tu. Lakini , Jee umeshawahi kujiuliza Valentine alikuwa
nani na wapi utamaduni huo wa siku ya Valentine umetoka na nini malengo
ya sikukuu hiyo? Mnamo karne ya tano Kanisa Katoliki lilitaka kumaliza
ukuwaji wa mila za wapagani ambapo Waroma walikuwa wakizifanya kila
mwaka tokea karne ya 4 BC.
Kutokana
na mila za za Waroma wakati huo, walikuwa wakifanya ndani ya siku ya
Februari 14 aina ya kamari maalum kuwashirikisha vijana wao wa kike na
wa kiume kwa ajili ya kupeleka zawadi kwa “mungu”wao Lupericus. Vijana
wa kike walishiriki katika kamari hiyo kwa kuweka majina yao kwenye
kiboksi na kasha la vijana wa kiume. Na vijana wa kiume huchagua majina
hayo. Kupitia kamari hiyo msichana aliyebahatika kuchaguliwa na mvulana
fulani, hapo huwa na mvulana huyo kwa mahusiano ya kimapenzi kwa kipindi
chote cha mwaka mzima hadi kamari ya mwaka unaofuata. Kanisa
halikufurahishwa kabisa na mpango huo wa kiibada za kiroma ambazo
hupelekea kufanya mapenzi kiholela kupitia kamari na likaamua kutokomeza
mila hiyo kwa kuchagua “Mpenzi ”, ambaye hutunukiwa badala ya mila ya
kamari ya “mungu” Lupericus. Kanisa likamchagua Askofu Valentine, mtu
ambaye alihukumiwa kuuwawa katika karne ya 3 AD kutokana na kukaidi amri
ya mtawala (Emperor Claudius). Mtawala ambaye alipiga marufu kuoa kwa
madai ya kuwa wanaume wanaoowa wanafanya vibaya vitani na wakati
mwengine huwa hawataki kuwacha familia zao na kwenda vitani. Askofu
Valentine alikuwa anawaalika wanaotaka kuoana na kuwaozesha kwa siri.
Kwa sababu hiyo akauwawa. Kabla ya kuuliwa alikuwa akituma ujumbe wa
kimapenzi kwa binti wa mlinzi wa jela aliyewahi kuwa na mahusiano nae
kimapenzi. Ujumbe wake ulikuwa: “kutoka kwa wako Valentine (from your
Valentine)”. Kwa hivyo Kanisa Katoliki likamchagua Askofu Valentine awe
mfano wa kuigwa kwa wapendanao na kutokemeza ibada za kipagani za
kufanya mapenzi kiholela kwa kuchagua mwanamke kwa
njia ya kamari. Na badala yake likahimiza kuowana. Lakini kutokana na
nidhamu ya kidemokrasia kuibuka katika nchi zao na watu kuwacha mafunzo
ya kidini na kuburuzwa na fikra za ‘uhuru’, siku hiyo ikawarejesha kule
kule katika zama za wapagani kwa kuhamasisha uchafu wa zinaa nje ya
ndoa. Mengi yanaweza kusemwa kutokana na utamaduni huo, lakini kuna
fikra moja msingi ambayo Waislamu wanapaswa kushikamana nayo. Uislamu ni
mfumo kamili wa maisha uliokamilika ambapo kwamba, chimbuko lake ni
Hukmu za Ki-Sheria. Hukmu hizo za kisheria ndio chanzo cha mila,
desturi, utamaduni na matendo ambayo Muislamu ameruhusiwa kuyafanya.
Kutokana na chanzo hicho (i.e Hukmu za Ki-sheria), Uislamu kwa uwazi
umeharamisha kushiriki katika Sikukuu zote za kikafiri, kama vile
kusherehekea sikukuu ya Valentine ambayo mwanzoni ilikuwa ya kipagani na
kisha ikaboreshwa tena katika sura tofauti na kanisa na pia sikukuu
nyengine zote. Uislamu kupitia Hukmu za Kisheria umeeleza kwa uwazi ni
zipi sikukuu za Kiislamu.
Imeelezwa kwamba, Anas bin Malik (ra) amesema:
“Wakati
Mtume (saw) alipokuja Madina, watu walikuwa wana skukuu mbili kutoka
katika masiku ya ujinga”. Yeye Mtume (saw) amesema: “Wakati nilipokuja
kwenu, mulikuwa na sikukuu mbili mulizokuwa mukisherehekea katika
kipindi cha ujinga. Allah (swt) ameziondoa na kuwapatia badala yake,
Skukuu ya kuchinja (Eid-l-adha) na Eid-el-Fitr. (Ahmad)
Kwa
hivyo, japokuwa kuna sikukuu nyingi katika ulimwengu lakini hizo ndio
sikukuu zetu Waislamu ambazo Allah (swt) ametuchagulia. Kuigiza mila na
vitendo vya kimagharibi ni mbinu ambayo makafiri hutumia kuwatumbukiza
Waislamu katika mwenendo usiokuwa wa kiislamu. Kila mara makafiri
wanafikiria jinsi gani wataweza kuwamaliza kabisa Waislamu, na kujaribu
kupanga mbinu mbali mbali ili kuweza kutimiza azma yao ya kuutokomeza
kabisa Uislamu. Katika jamii tunayoishi leo, kwa bahati mbaya, dhana ya
mchanganyiko usiokuwa na mipaka baina ya wanawake na wanaume ni jambo
linalopigiwa debe na makafiri na kupandikizwa katika mabongo ya Waislamu
ili lionekane kuwa ni jambo la kawaida, na kututaka tuzikubali fikra
zao hizo kwa kisingizio chao kwa kuwa sisi ni sehemu katika jamii yenye
mila mchanganyiko (Multicultural Society).
Inafaa
tuelewe kwamba umma wa Kiislamu unatakiwa uwe makini na kutambua mbinu
hizo za makafiri, ili tuweze kuhuisha na kushikamana na uelewa wetu juu
ya miondoko yetu ya kimaisha kama ilivyopokelewa kutoka katika Qur-an na
hadithi za Mtume (Saaw). Uislamu wetu umeweka wazi juu ya jinsi gani
Waislamu waishi maisha yao baina ya wanawake na wanaume, mahrim na
wasiokuwa mahrim, katika maisha ya ndani (Private live) na maisha ya nje
(Public life)nk.
Sikukuu
ya Valentine ni moja ya mifano, ambapo mahusiano nje ya taasisi ya ndoa
si tu huruhusiwa bali pia huhimizwa.Vyombo vya habari pamoja matangazo
mbali mbali hupigia debe mahusiano hayo hasa katika sikukuu hiyo. Ni
ukiukaji wa Sheri’a ulioje, ambapo mila hizi za kidemokrasia huwafanya
vijana kuchanganyikiwa na kukimbilia mahusiano hayo kwa kutafuta kuwa na
mpenzi hususan inavyohimizwa na sikukuu hiyo.
Takriban
ulimwengu nzima, mashule, vyuo, vilabu vya usiku zimo katika maandalizi
ya sherehe hizo za skukuu ya wapendanao. Pia kwa bahati mbaya
huwajumuisha baadhi ya Waislamu waliochanganyikiwa katika matukio hayo
ya michanganyiko ya jinsia tofauti kwa jina la mchanganyiko wa
kimapenzi. Jambo linaloonesha namna baadhi ya Waislamu walivyokuwa mbali
na fikra yao safi ya kiislamu na hatimaye kukumbatia fikra na mila za
kikafiri.
Ni
vigumu kufikiria kile ambacho kanisa katoliki kilitaraji kukifikia kwa
kutaka kuhifadhi taasisi ya ndoa na kuzipinga mila za kipagani na
kuanzisha siku ya Mtakatifu Valentine! Hawakulifikia hilo kwa kuwa
Ukiristo sio mfumo wa maisha na hivyo kimaumbile hauna nguvu na ujasiri
isipokuwa kusalimu amri kwa nidhamu ya kidemokrasia.
Na badala yake leo tunaona mahusiano ya kiholela ya kimapenzi yamerudi tena na yamezidi katika jamii, na sikukuu
hii ya Valentine imekuwa ndio kichocheo kikubwa ambayo matokeo yake ni
uzinifu, mimba nje ya ndoa, na utoaji wa mimba na yote yanayopelekea
kuporomoka kwa maadili na kupoteza utukufu/ heshma ya jamii. Jee huo
ndio ujumbe tunaotarajia kuwafikishia watoto wetu kutoka katika siku
hii?
Katika
Uislamu mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanamke na mwanamume
yameelezwa wazi wazi na Sheria kupitia utaratibu maalumu ambao ni ndoa.
Ibn Masoud amesema kuwa. Mtume (saw) amesema:
“Enyi makundi ya vijana, yeyote mwenye uwezo wa
kuoa na aoe kwani jambo hilo litamsaidia kuinamisha macho yake, na
itamuhifadhia sehemu zake za siri kutokana na uchafu wa zinaa. Na
asiyeweza kuoa basi na afunge kwani hiyo itakuwa ngao kwake”.
Hukmu
za kisheria zinahakikisha kuwa jamii iliyosimama juu ya misingi hiyo
itakuwa mbali na uzinifu wa kiholela na itakuwa na mwamko wa kimaadili.
Mambo ambayo waziwazi yamekosekana katika jamii za kimagharibi na kwa
bahati mbaya tunayaona yanafikishwa katika ardhi za Kiislamu pia.
Sheri’a
inatambua mahitaji na hisia ya kimaumbile ya matamanio waliyonayo
wanawake na wanaume na ndio maana zikaweka taratibu maalum katika
kuzishibisha ghariza/hisia hizo na mahitaji hayo katika utaratibu ambao
mwanadamu atapata utulivu bila ya kudhurika.
Sisi
Waislamu tunapaswa kufahamu kwamba matendo yetu yote lazima yafuatane
na Hukmu za Kisheria ikiwa ndio chanzo kitukufu cha mwongozo kwetu sisi.
Aidha ikiwa ni kwa vitu vidogo vidogo au kwa maamuzi makubwa, katika
maisha ya ndani (private) au ya nje (public), tunalazimika kutenda baada
ya kufahamu kile alichokiteremsha Allah (swt) juu ya suala husika.
Vyenginevyo
tutaingia katika makucha ya mafisadi, kama vile uhuru, demokrasia,
michanganyiko ya jinsia tofauti pamoja na maslahi binafsi. Vile vile
ikiwa tutachukua taratibu zisizokuwa za kiislamu katika maisha yetu, kwa
ajili ya kuwaridhisha wale waliotuzunguuka, lazima tufahamu kuwa
kufanya hivyo kutatufanya tuwe madhalili na starehe zao zitakuwa pigo
kwa dini yetu.
Allah (swt) anasema:
“Hawataridhia Mayahudi na Manaswara mpaka mfate mila zao…”(TMQ 2:120).
Wakati
umefika tuwe macho Waislamu na mbinu za makafiri, iwe katika michezo
yao (movies), vitabu vyao vya hadithi, sherehe zao nk. Malengo makubwa
ambayo wameyaficha makafiri katika vifua vyao yana athari mbaya kwa
ummah wa kiislamu. Ni wakati wa kuamka na kutafuta dola yetu (Khilafah)
katika ulimwengu ili tuonje ladha ya Uislamu kivitendo na kukomesha mila
na sherehe potofu za kikafiri.
No comments:
Post a Comment