Padre FESTO TINGO
Wa parokia ya KENI ROMBO JIMBO LA MOSHI alipokuwa katika maazimisho ya misa takatifu
ya mazishi ya mzee HONORATH MASSAWE
katika kijiji cha MACHAME ALEN ROMBO
akitoa tafakari ya ne la Mungu liliosomwa katika ibada hiyo aliwaasa wakrisu
kwa mambo mengi sana. kama tulivyokuandalia hapo chini
1.
Padre FESTO
TINGO aliwataka wakristu kumtafuta kristu wakati wa uhai wao na ndugu kama
tunapendana hebu tuonyeshe upendo huo mtu akiwa hai, na kama tunataka siku ya
mwisho apate heshima basi tumuaandae mapema kupata heshima na ndgugu tuhusike
kwa kiwango kikubwa kuwa kuitafuta heshima hiyo ya wapendwa wetu wakati wa uhai
wao. Mfano:- unakuta mtu hakuwa mkristu hai lakini siku akifa tunataka apewe
heshima ya maziko ya kikristu kitu ambacho siyo sawa, maziko ya kikkristu
anapewa mkristo aliyejitambua na kumtafuta wakati wa uhai wake. Haina msaada
kumlazimishia mtu kuwa mkristo wakati yeye hakuutafuta ukristu hata kama
akifanyiwa maziko hayo hamna kitu
2. Wakristu kuuishi vyema ukristu. Tunapaswa
kutambua kuwa kanisa katoriki lina utaratibu wake ili kuwa mkristu hai ikiwa ni
pamoja na kuwa na sakramenti zote anazositahili
mkristu kushirikiana na wenzake kuanzia
kwenye jumuiya mpaka parokiana. Na siyo siku ya mwisho watu kulalamika kuwa
kanisa halijamtendea haki marehemu ili hali yeye alikuwa halitendei haki
kanisa. Ukweli utabakia kuwa pale pale kama mtu hakumtafuta mungu wakati wa
uhai wake asilazimishiwe akiwa amekufa kwani mazishi ya siku ya mwisho
hayatamsaidia chochote.
3. MUNGU HATATOA HUKUMU SIKU YA MWISHO
Mungu hatahukumu mtu siku ya mwisho bali
kila mtu amekwisha kujihukumu mwenyewe akiwa huku duniani siku ya mwisho kazi
ya mungu itakuwa nyepesi sana kwani yeye atakuwa akitekeleza hukumu ya kila
mmoja aliyochagua. Kwani kama ni kwenda mbiguni mtu anatengenenza njia yake
mwenyewe akiwa hapa duniani na kama ni kwenda motoni mtu anajichagula mwenyewe.
Je? wewe umekwisha kujihukumu au bado.
4. POMBE SIYO HARAMU WANAO AMINI KUWA POMBE NI
HARAMU WAMEFILISIKA KIMAWAZO.
Wanao amini kuwa pombe ni haramu wamefirisika
kimawazo. Na pombe siyo shetani kama watu wengi wanavyoamini wala siyo mbaya
kama watu wanavyofikiri. Padre Festo Tingo aliwauliza waumi swali jepesi je?
Shetani ni nani,kitu haramu ni kipi,au kitu kibaya ni kipi, waumini wakajibu ni
chochote kile kinachofanyika kinyume na mapenzi ya munu (kinachotenda dhambi ) ok baada ya jibu hilo akauliza tena ni lini
umewahi kukuta kreti la Kilimanjaro, safari, au caster likitenda zambi au
konyagi ikivunja amri yoyote ya mungu au harken ikipigana na dompo jibu hakuna.
Ok sasa kama jibu ni hakuna shetani ni wewe ambaye unakunywa pombe mpaka
inakutawala badla yaw ewe kuitawala au ni pombe, shetani ni wewe unayepigana na
kuvunja amri nyingi za mungu baada ya kunywa pombe au ni pombe? ‘’mimi mwenyewe
sinywi lakini siamini kuwa pombe ni haramu na ninaweza kunywa muda wowote ule
kwani ni kinywaji kama vinywaji vigine haramu ni nyie watumiaji mnaotawaliwa na
pombe’’ hayo yalikuwa maneno ya padre Festo je wewe unasemaje POMBE NI HARAMU
AU SIYO HARAMU? Tupia comenti yako hapo
No comments:
Post a Comment