Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria
na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club
inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka,
mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin
Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Aisha Mashauzi.
Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006,
Wema Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny
Love. WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli
hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria
kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata
nafasi ya kujitetea (balansi).
Asha Baraka.
“Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City,
Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya
kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama
mnavyofanya magazetini. “Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema
maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua
kushughulika na Mpoki na si mwingine,” kilisema chanzo hicho. Maimartha
wa Jesse. MADAI YAO YA MSINGI
Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao-
kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo
ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu
wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa
kuliko zote Afrika Mashariki. KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao
linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka. MAI;
aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini
akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya
mwonekano. RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani.
Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu
Hans.
Wema.
KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha
akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi! VANESSA; alimwambia
afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si
vyema kuyaandika hapa).
No comments:
Post a Comment