MWACHENI Diamond
aitwe Diamond! Hiyo kauli pekee unayoweza kuisema kufuatia wakali wa
muziki wa R&B kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye ‘P-Square’
kuukubali uwezo wa kimuziki wa bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ijuma Wikienda linakupa mchapo hatua kwa
hatua.
Bwa’mdogo kutoka Tandale, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa madansa wake ndani ya Lagos, Nigeria.
NI LAGOS, NIGERIA
Wakali hao walionesha
kumpigia saluti Diamond baada ya kukutana naye kwenye tamasha la utoaji
wa Tuzo za Wanamichezo Bora Afrika lililofanyika Lagos, Nigeria, usiku
wa kuamkia Januari 9, mwaka huu.
WALIANZIA HOTELINI
Kwa mujibu wa chanzo
kilichoambatana na Diamond nchini humo, saa chache kabla ya shoo kuanza,
P-Square walimuibukia kwenye Hoteli ya Eko aliyofikia jijini humo na
kummwagia pongezi nyingi sambamba na kumshauri baadhi ya vitu vya
kimaendeleo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo hicho kilisema,
P-Square walionekana kuvutiwa zaidi na juhudi binafsi za Diamond kiasi
cha kuweza kuipeperusha bendera ya Afrika Mashariki katika levo za
kimataifa.
“Jamaa walipomuona tu
hotelini waliguswa sana na juhudi zake binafsi maana wanatambua jinsi
gani muziki ulivyokuwa mgumu kuuvusha nje ya nchi yako lakini kwa kuwa
Diamond ameweza, walimpigia saluti,” kilisema chanzo hicho.
ARUHUSIWA KOLABO
Chanzo hicho kilizidi
kumwaga data za ndani kwa kusema, mbali na kumpigia saluti, P-Square
walionesha wako tayari kumsapoti Diamond kwa kumpa nafasi ya kufanya nao
kazi yaani kolabo.
“Wamempa nafasi ya
kufanya naye kazi pale atakapojisikia kutokana na mipango yake, kama
akiamua kufanya sasa au baadaye ni uamuzi wake lakini jamaa (P-Square)
hawana kinyongo naye lengo lao ni kuona muziki wa Afrika unateka dunia,”
kilisema chanzo hicho na kuongeza:
‘Diamond Platnumz’ akiwa na Paul Okoye wa 'P Square'.
“Walimwambia the way (namna) alivyo na juhudi kwenye kazi yake
anatambulika Nigeria utafikiri ni msanii kutoka Nigeria, walimpa mbinu
zao za namna walivyopigana hadi kufika hapo walipo.”
MASTAA WAMUIBUKIA
Mbali
na P-Square, mastaa mbalimbali wa Nigeria walimuibukia Diamond hotelini
hapo akiwemo Mr Flavour na Jude Abaga ‘M.I’, ambao walimpa pongezi
Diamond kwa kujua kumiliki vyema jukwaa kwani wamekuwa wakifuatilia shoo
zake hasa anapotupia video zake mitandaoni.
APIGA SHOO YA MAANA
Ulipofika wakati wa
kupanda jukwaani, Diamond aliitikisa Nigeria kwani alionesha vitu vya
tofauti wakati akiimba nyimbo zake na kuwafanya Wanigeria na waalikwa
mbalimbali wapigwe na butwaa huku wengi wakiishia kumpigia makofi na
shangwe la kufa mtu.
DIAMOND ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu
alimcheki Diamond kupitia mtandao wa WhatsApp ambapo aliwashukuru mastaa
hao wa Nigeria kwa upendo wao na kuahidi kuendelea kufanya maajabu
zaidi katika levo za kimataifa.
“Wana wamenisapraizi
hotelini, tumepiga stori nyingi, wameonesha wanakubali kile ambacho mimi
nafanya, jukwaani nimefanya vizuri, watu na heshima zao mwishoni
walipiga makofi kuonesha wamekubali.
KUHUSU KOLABO?
“Kuhusu kolabo na
P-Square, ni mapema sana kuzungumzia kwa kuwa nina mipango mingi ya
kufanya mwaka huu, mashabiki wakae mkao wa kula, nikiona inafaa,
nitafanya nao maana wao hawana shida na mimi,” alisema Diamond.
P-SQUARE NI ZAIDI YA DAVIDO
Awali, kabla Diamond
hajakutana na P-Square, alishirikiana na mkali mwingine wa Nigeria,
Davido katika wimbo wake wa Number One Remix ambaye inaaminika kwa
umaarufu na uwezo wa kimuziki yupo chini ya P-Square.
No comments:
Post a Comment