FUMANIZI HATARE:SERENGETI BOY AFUMANIWA LIVE GESTI NA MKE WA KIGOGO
KABAANG! Kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa
Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo
mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.
Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo.
Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu
iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba
anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana
huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa
kuserebuka.
“Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika
gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa
tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu
na kuongeza:
“Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke,
walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.
Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza
kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa
pesa hizo.Barua ya makubaliano ya kulipwa pesa kwa kigogo huyo shilingi laki tano.
Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya makubaliano
jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na iwe kama
fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu.
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na kudai
ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu.
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya kwani
ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi wa
mtaa huu nitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi za
kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.
No comments:
Post a Comment