Mwigulu Nchemba ahitimisha ziara yake mkoa wa Mara kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja serengeti.
Katika mkutano huo ambao Mwigulu aliambatana na Mbunge wa
Tarime kwa tiketi ya CHADEMA Mh.Easter Matiko ambaye kwa nafasi yake
aliwaambia wananchi serikali ya magufuli na mawaziri wake wanaonesha
mfano wa kufanya kazi bila kunagua vyama,Kitendo cha waziri kufika
katika jimbo hili na kuzungumza na wananchi ni dhahiri umoja unakwenda
kutamalaki.
Akizungumza na wananchi wa Tarime mjini,Mwigulu chemba
amewaambia wanatarime kuwa,mnada wa ng'ombe Magena unafanyiwa upembuzi
ili serikali ijiridhishe na ama uendelee kufanya kazi au uhamie Kirumi.
Mbali na mnada huo,Mwigulu amewaeleza wanatarime kuwa
wizara yake imejipanga kuboresha mfumo wa usambazaji wa pembejeo kwa
wakulima,mfumo ambao utahakikisha wakulima kwa silimia kubwa kama sio
wote wanapata fursa ya kunufaika pembejeo zenye ruzuku ya serikali.
Kwa upande wa ufugaji,Nchemba anasema,"huu ni muda muafaka
kwa wafugaji kuachana na kufuga mifugo mingi isiyo na tija
kubwa,nimeongozana na wataalamu ambao wanaandaa utaratibu wa kuwapatia
wafugaji elimu na maeneo ya kufuga kwa kisasa "mifugo michache,tija
kubwa".
No comments:
Post a Comment