Hii Ndio Sababu ya Clouds FM kushindwa Kumtumia Diamond Kwenye Show zao za Fiesta.
Wakati wasanii wakibongo kwa ujumla wao
wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu, Diamond ameendelea
kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi cha jamaa wa Clouds
Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu kwenye show zao!
Ieleweke kwamba kipindi hiki huwa ni cha
neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine hufikia kuomba angalau tu
wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani kuonana na mashabiki.
Diamond kwa kipindi kirefu sasa amekuwa
ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje ya nchi kiasi kwamba
imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki show za hapa.
Pamoja na upizani mkubwa mno naoupata
kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata kwa wale ambao bado
walikuwa wabishi kumkubali Diamond.
Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumtakia
mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi makubwa kabisa
kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.
No comments:
Post a Comment