Wednesday, October 22, 2014

Mambo 10 Usiyojua Kuhusu Vatican.




1. Ni nchi kamili yenye mamlaka kamili. Ina mfumo wake wa posta, fedha na ulinzi.
2. Iko ndani ya mji wa Roma kwenye nchi ya Itali,
3. Utawala wa Vatican ni wa kidini na mkuu wa nchi ni papa.
4. Vatican imezungukwa na ukuta.
5. Ni nchi yenye watu wachache zaidi duniani. Ina wananchi wapatao 800, wengi wao ni viongozi wa kidini.
6. Asilimia kubwa ya wananchi wa Vatican wanaishi nje ya nchi, kama mabalozi na wawakilishi.
7. Kuna jeshi maalumu la ulinzi linaloitwa Swiss guard, wanajeshi wake wana uwezo mkubwa sana.
8. Ni nchi yenye eneo dogo zaidi, takribani ukubwa wa hekari 100.
9. Vatican haina mfumo wa kodi.
10. Kuna njia ya siri ya papa kutoroka ikiwa kuna tatizo la usalama.

No comments:

Post a Comment