Vijana wametakiwa kulinda nguvu ya Taifa ikiwa ni pamoja na kufanya mapinduzi na maamuzi ya kweli ili kuweza kupata viongozi na si kuchagua viongozi mizigo ambao watachosha wananchi na kufuja mali za umma
Kauli hiyo Mratibu wa uhamasishaji wa
vijana Chadema Taifa Edward Simbey katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivi
karibuni katika mji mdogo wa Utegi
wilayani Rorya Mkoani Mara katika mwendelezo wa ziara ya kuelimisha
wananchi kuhusu chaguzi za serikali za mitaa pamoja na maoni juu rasmu ya
katiba mpya huku wakiambatana na viogozi
wa kitaifa Balaza la akina Mamakupitia Chama Cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA
chini ya Mwenyekiti akina Mama Bawacha Taifa Halima Mdee.
Edward alisema kuwa taifa lolote duniani
vijana ndo nguvu kazi ya taifa katika chachu ya kusukuma gurudumu la Maendeleo
ikiwemo na wilaya ya Rorya.
Aidha Mratibu wa vijana aliwataka vijana hao Vijana
waoneshe nguvu ya jeshi ili kuwepo upambanaji wa kweli mpaka haki inapatikana
huku akilaani jeshila polisi kuondokana na kunyanyasa vijana na kuwageuza
mitaji na kuwatengenezea kesi zisizokuwa za msingi ili kuweza kujipatia
maslahi.
Kwa upande wakeMbunge wa Viti maalumu
Ester Matiko ambaye pia ni Mwenyekiti akina Mama Mkoa wa Mara alisema kuwa akina mama hospitalini wamezidi
kuangaika na kununua madawa wakati serikali inazidi kutumia fedha kubwa katika
mambo yasiyo ya msingi.
“Wanafunzi sasa wanatahabika kwa
kukosa Madawati, Madarasa yanadodondoka
kwanini nhizo fedha serikali inazoharibu zisije kujenga shule na kununua
madawati” alisema.
Naye katibu wa Mkoa mkoa wa Mara Chacha Heche
amezidi kulaani viongozi wanaotumia ubabe kunyanyasa wananchi kuondoka na vitendo hivyo mara moja.
Hata hivyo meya wa manispaa ya musoma
Alex Kisurula alisema kuwa alisema kuwa
maendeleo yanletwa na viongozi wenye uzalendo pamoja na siyo viongozi
wanaojitapa kwa utajili walionao wakati wananchi wanazidi kutaabika.
Maisha yangu yanfanana na wananchi wa
ngu lakini nyie wananchi wa Rorya maisha mbunge wenu yanafanana na ya kwenu
alisema meya.
Pia meya huyo aliwataka wananchi wa
rorya kuondokana na vijazawadi wanavyopatiwa
na kubadilisha mawazo katika kupiga kura na kuchagua viongozi wabovu.
No comments:
Post a Comment