Mzee Nestory Karani Malima alizaliwa tarehe 28/12/1924 na amefariki tarehe 11/08/2018 akiwa na miaka 94. marehemu mauti yalimkuta akiwa katika hosipitali ya wilaya ya tengeru mkoani arusha alipokuwa akipatiwa matibabu , Marehemu alikuwa akiuguzwa na binti yake Sabina Gidembu ambaye anakaa Arusha. katika maisha ya uhai wake marehemu ameacha alama kubwa sana katika kijiji cha usagara na vijiji vya jirani kwani katika historia marehemu ndiye aliyeanzisha ukatoriki katika kijiji cha usagara na kutafuta eneo la kujenga kanisa na hakuishia Saragana tu aliendelea kutoa mafundisho ya dini kwa vijiji vya jirani. Hakika mzee Nestory alikuwa taa kawa wengi na amewawashia wengi mwanga.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA ,
NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE ,
APUMZIKE KWA AMANI
AMINA.